HabariMilele FmSwahili

Wafanyikazi Bomet kususia kazi endapo hawatalipwa mishahara yao

Wafanyakazi 8,000 katika kaunti ya Bomet wameapa kususia kazi endapo hawatalipwa mishahara yao ya miezi miwili kufikia leo jioni.
Mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi hao Jesca Langat anasema ilani waliyotoa inakamilika leo na hawatafutilia mbali mgomo huo.Akiwahutubia wanahabari mjini Bomet, anasema wafanyakazi hao wanadai jumla ya shilingi millioni 200 . Bi Langat aidha amelalamikia kile anachokitaja kama kuwepo kwa ubaguzi katika utoaji malipo huku akiitaka serikali ya kaunti kuheshimu haki za wafanyakazi wake.

Show More

Related Articles