HabariPilipili FmPilipili FM News

Mgombea Ugavana Mombasa Ataka Ulinzi Zaidi.

Mgombea kiti cha ugavana kwa tiketi ya chama cha VDP Hezron Awiti ameitaka serikali kumpatia ulinzi wakutosha wakati huu wa kampeni za kisiasa.

Akiongea hapa mjini Mombasa wakati wakuthibitisha kubomolewa kwa bango lake la kampeni eneo la buxton awiti amedai kuhitaji ulinzi zaidi kutoka kwa serikali ili kuwa na uhuru wakufanya kampeni yake popote pale katika kaunti ya Mombasa.

Akikariri kilichotokea mwaka 2013 ambapo amedai alifanyiwa jaribio la kuuawa mgombea huyo amesema mpaka sai hakuna  ukweli wa kisa hicho hivyo kuhimiza maafisa wa polisi kukamilisha uchunguzi na kutaka walinzi zaidi.

Kauli ya Awiti inajiri wakati ambapo joto la kisiasa limepamba moto huku zikiwa zimebaki siku 24 kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika nchini.

Show More

Related Articles