HabariMilele FmSwahili

NASA yalalamikia utovu wa usalama Lamu na Kaskazini Mashariki

Muungano wa NASA umelalamikia utovu wa usalama katika kaunti za Lamu na Kaskazini Mashariki. Makatibu wa vyama tanzu vya NASA wanaitaka serikali kuimarisha usalama maeneo hayo wakisema hali hiyo huenda ikaathiri uchaguzi mkuu. Katibu wa ANC Godffrey Otsotsi anasema ni jukumu la serikali kuwatuma walinda usalama zaidi kukabiliana na wanamgambo wa Al shabab. Mohammed Gulleid wa CCM amelaani vurugu zinazoshuhudiwa katika mikutano ya kisiasa na kuwataka vijana kutokubali kutumiwa na wanasiasa. Yakijiri hayo,katibu wa ODM Agnes Zani amewataka wananchi katika ngome za NASA kutokubali kupeana vitambulisho vyao.

Show More

Related Articles