HabariMilele FmSwahili

Wavinya Ndeti kushiriki uchaguzi bila vikwazo

Mgombea wa ugavana kaunti ya Machakos kupitia chama cha Wiper Wavinya Ndeti atashiriki uchaguzi wa Agosti nane bila vikwazo. Hii ni baada ya mahakama ya rufaa kudinda kumzuia kuwania kiti hicho kufuatia rufaa iliyowasilishwa na mwakilishi wadi aliyekuwa akipinga uamuzi wa mahakama kuu uliomruhusu kuwania. Wakati huo huo mahakma hiyo pia imetupilia mbali mashtaka ya ufisadi dhidi ya aliyekwua waziri wa uchukuzi Michale Kamau. Majaji wanasema tume ya ufisadi haikuwa imebuniwa ipasavyo wakati wa kumshtaki.

Show More

Related Articles