HabariPilipili FmPilipili FM News

Ombi La Makasisi Kwa Gavana Kingi.

Zaidi ya makasisi mia 200 kutoka madhehebu mbali mbali eneo bunge la Ganze kaunti ya Kilifi wamemtaka gavana wa kaunti hiyo Amason Kingi, kuwashirikisha katika serikali yake ya kaunti iwapo atafanikiwa kurejea mamlakani baada ya uchaguzi.

Akiongea kwenye kikao na makasisi hao kilichoandaliwa eneo la  Matano Mane, katibu mkuu wa chama cha makasisi pwani Bishop Amos Lewa, amesema kuwakilishwa kwao katika serikali ya kaunti kutasaidia kutatua changamoto zinazoathiri jamii na makanisa  yao kwa ujumla.

Wamemuomba gavana kingi kushughulikia changamoto ya wao kutozwa ada za viwanja na shirika la NEMA pamoja na serikali ya kaunti hiyo pale wanapo fanya mikutano ya injili.

 

Show More

Related Articles