HabariPilipili FmPilipili FM News

Vita Vya Mabango Vya Rindima Mombasa.

Mzozo wa mabango ya kampeni kwa wanasiasa umechukua mkondo mpya mapema leo baada ya bango la mwaniaji wa kiti cha ugavana kaunti ya Mombasa kwa tiketi ya vibrant democratic party Hezron Awiti kuangushwa na watu wasiojulikana eneo la buxton usiku wa kuamkia leo

Akiongoa na waandishi wa habari Awiti amemlaumu gavana wa sasa Ali Hassan Joho ambaye ni mpinzani wake mkuu, kwa kile alichokitaja kama kumtishia ili asiangike mabango yake ya kampeni.

Walioshuhudia kisa hicho wamesema waliona vijana waliokuwa na mapango kwenye gari aina ya probox ambao walihusika kuliangusha bango hilo.

Kisa hiki kinakuja wiki chache baada ya bango hilo katika eneo la buxton kung’olewa na askari wa kaunti, kwa kuwa  bango hilo liliangikwa bila idhini ya serikali ya kaunti.

Show More

Related Articles