HabariMilele FmSwahili

Moi atuma risala zake kwa familia ya balozi Kiplagat akimtaja kama mzalendo

Rais mstaafu Daniel Moi amemtaja aliyekuwa mwenyekiti wa tume ya ukweli haki na maridhiano Bethuel Kiplagat kama mzalendo aliyejitolea kuhudumia taifa.katika risala zake kwa familia ya balozi kiplagat ambaye amefariki mapema leo baada ya kuugua kwa muda mrefu, Moi anasema upendo aliokuwa nao kwa taifa, ilimfanya kuendeleza jitihada za kidiplomasia ndani na nje ya taifa. Mwenyekiti wa baraza la magavana Josphat Nanok pia ameelezea kutamaushwa na kifo chake Kiplagat. Amemtaja kama mmoja wa viongozi waliojitolea zaidi kuhakikisha taifa linakuwa na amani.

Show More

Related Articles