HabariMilele FmSwahili

Matiangi kukutana na wakuu wa shule za sekondari na msingi

Waziri wa elimu Dkt Fred Matiangi atakutana na kushauriana na wakuu wa shule za sekondari na wale wa shule za msingi. Ni mkutano ambao unalenga kuangazia mipango ya wizara yake kwa ajili ya mitihani ya kitaifa ya mwaka huu. Ni mkutano ambao pia utawahusisha wakuu wa elimu nchini. Haya yanajiri huku ripoti zikiashiria kwamba tayari mitihani hiyo ya KCPE na KCSE imechapishwa. Wanafunzi milioni 1.6 wanatarajiwa kufanya mitihani hiyo mwaka huu, ikitarajiwa kutakua na masharti magumu zaidi kuzuia wizi wa mitihani.

Show More

Related Articles