HabariMilele FmSwahili

Balozi Bethuel Kiplagat aaga dunia

Aliyekuwa mwenyekiti wa tume ya ukweli haki na maridhiano balozi Bethuel Kiplagat amefariki. Kiplagat amefariki mapema leo asubuhi katika hospitali ya Nairobi ambako amekuwa akitibiwa. Balozi Kiplagat atakumbukwa zaidi kutokana jitihada zake za kueneza amani nchini, kuu ikiwa ni kuongoza tume ya TJRC ambayo ilihusika pakubwa katika kuangazia dhulma za kihistoria. Kiplagat pia alituhumiwa kuhusika na mauaji ya Wagalla kaunti ya Wajir mwaka wa 1984 ambapo watu 4000 waliuwawa, hatua ambayo ilimsababishia changamoto kadhaa akihudumu kama mwenyekiti wa tume hiyo. Hata hivyo alikana na kujitetea alihusika pakuwba kuleta amani.amefariki akiwa na miaka 81.

Show More

Related Articles