HabariMilele FmSwahili

Thuo Mathenge kujua hatma yake na IEBC Alhamisi ijayo

Mgombea ugavana kaunti ya Nyeri Thuo Mathenge ambaye aliondolewa kwenye kinyang’anyiro hicho na tume ya uchaguzi IEBC sasa atajua hatma yake siku ya Alhamisi juma lijalo. Hii ni baada ya mawakili Kioko Kilukumi anayemwakilisha Thuo na Victor Obondi wa IEBC kuwasilisha hoja zao mbele ya jaji mkuu Abigael Muchira. Wakili Kilikumi aliambia mahakama kuwa Thuo hakupewa nafasi ya kujitetea mbele ya kamati ya tume ya IEBC akisema kuwa alinyimwa haki ya kujitetea. Hata hivyo Obondi aliitetea tume ya IEBC akisema tume hiyo haikuhitaji kumpa nafasi kujielezea.Thuo alipokonywa tiketi yake hata baada ya kupitishwa kwa madai kuwa hajahitimu kimasomo kuwania kiti cha ugavana.

Show More

Related Articles