HabariMilele FmSwahili

Wakimbizi wa ndani kwa ndani Kisii kupata fidia

Wakimbizi wote wa ndani kwa ndani kaunti za Kisii na Nyamira watapata fidia yao kama ilivyoahidi serikali ya Jubilee. Naibu rais William Ruto anasema japo kumekua na mzozo kuhusiana na wakimbizi halali wanaopasa kupata ridhaa hiyo,serikali imeweka mikakati kuhakikisha zoezi hilo linakamilishwa haraka. Akiwahutubia wenyeji maeneo tofauti kaunti hizo,Ruto amesema lengo la serikali ni kuhakikisha wakimbizi wote wanapata makao kabla ya Agosti nane.Aidha naibu Rais ameendelea kumshtumu upinzani kwa kutatiza juhudi za taifa kuwa na uchaguzi Agosti nane. Ruto amewataka wakenya kuwapuuza wapinzani wao akisema hawana ajenda yeyote.

Show More

Related Articles