HabariMilele FmSwahili

Mkutano wa NASA mjini Thika watibuka

Mkutano wa kujipigia debe ulioandaliwa na vigogo wa NASA mjini Thika umetibuka baada ya vijana kuuvuruga. Inadaiwa vijana hao hawakufurahishwa na semi za wana NASA wakiongozwa na mgombea urais Raila Odinga dhidi ya kushtumu uongozi wa serikali. Polisi wamelazimika kutumia vitoa machozi kuwatawanya vijana hao walioanza kurusha mawe katika eneo la mkutano.Hali hiyo pia ilishuhudiwa eneo la Kenol kaunti ya Murang’a pale vijana wenyeji walipodinda kuhutubiwa na seneta Johnston Muthama.Hata hivyo,Raila alifanikiwa kuwahutubia huku akiwoamba kuunga mkono azma yake kuliongoza taifa alivyofanya mwaka 2002 alipofanya kazi na rais mstaafu Mwai Kibaki.

Show More

Related Articles