HabariMilele FmSwahili

IEBC yatupilia mbali kesi iliyowasilishwa na Florence Kajuju dhidi ya mpinzani wake

Tume ya IEBC imetupilia mbali kesi iliyowasilishwa na mwakilishi wa kina mama kaunti ya Meru Florence Kajuju dhidi ya mpinzani wake Kawera Mwangaza kwamba anatumia kituo kimoja cha runinga kumchafulia jina kwa misingi ya kukosa ushahidi wa kutosha. IEBC kupitia naibu mwenyekiti wake Consolata Maina imesema ushaidi uliotolewa haukuonyesha kwamba matangazo yanayopeperushwa na kituo hicho yameshawishiwa na bi Mwangaza. Kamati hiyo aidha imeshauri kwamba bi Kajuju ako huru kuishtaki runinga ya Baite kwa kumchafulia jina.

Show More

Related Articles