HabariPilipili FmPilipili FM News

Kiwanda Cha Nyama Cha Karabatiwa Mombasa.

Kiwanda cha nyama cha Kibarani kinawahimiza wakazi kuweza kununua nyama huko ili kukipa hadhi kiwanda hicho baada ya kiwanda hicho kufanyiwa ukarabati.

Akiongea na wanahabari mwenyekiti wa kiwanda hicho nchini  Joseph Learamo amesema kuwa serikali kuu iliweza kutoa kima cha bilioni 3.4 ili waweze kufanya ukarabati wa viwanda vyote vya nyama nchini.

Aidha Learamo amesema kuwa licha ya kiwango cha utalii kushuka kwa kiwango kikubwa, utalii wa watu nchini umewafanya kuweza kuuza nyama kwenye hoteli hapa Mombasa na Nairobi

Vilevile ameongeza na kusema kuwa kiwanda hicho kitakuwa kinachinja kati ya ng’ombe 100 hadi 150 kwa siku na kurai serikali ihakikishe kuwa kila idara ya serikali inaweza kununua nyama kwenye kiwanda hicho ili kiweze kufanya biashara na serikali.

Show More

Related Articles