HabariPilipili FmPilipili FM News

Serikali Yatakiwa Kuwakabili Wanaoficha Unga Wa Mahindi.

Wakazi wa kaunti ya Mombasa wamezidi kulalamika kutokana na ukosefu wa unga madukakani, baadhi ya wenye maduka wakisusia kuuza bidhaa hiyo.

Wachache wamasema hupata unga huo wa serikali kwa bei ya juu zaidi.

Wakizungumza na meza yetu ya habari,wakazi wa eneo la Changamwe wamelaumu serikali kwa kutoingilia kati na kuona kuwa wananchi wanafaidika na bidhaa hiyo muhimu.

Wakati huo huo wakazi wa eneo la Migadini wameelezea hofu kuwa  baadhi ya unga umefichwa na  baadhi ya watu aidha wengine wamesema unga huo hutolewa tu kwa baadhi ya maduka.

 

Show More

Related Articles