HabariMilele FmSwahili

Watu 6 watekwa nyara eneo la Milihoi, Lamu

Watu 6 akiwemo afisa mmoja mkuu wa serikali wametekwa nyara eneo la Milihoi kaunti ya Lamu. Inashukiwa wote hao wametekwa nyara na waasi wa Alshabab katika barabara kuu ya Lamu kuelekea Mpeketoni. Walioshuhudiwa wakitekwa wanasema waasi zaidi ya thelathini waliwafumania watu hao wakiwa katika msafara uliokuwa ukielekea eneo la witu kutembelea familia za wale ambao wametoroka kutoka msitu wa Boni kufuatia oparesheni ya kuwaondoa waasi wa Alshabaab. Mkuu wa polisi pwani James Akoru amedhibitisha.

Show More

Related Articles