HabariMilele FmSwahili

Ikulu ya rais yapuuza madai ya Raila kwamba Jubilee haitokubali matokeo ya uchaguzi

Ikulu ya rais imepuzilia mbali madai yaliotolewa na mgombea urais wa NASA Raila Odinga kwamba Jubilee inapanga kutokubali matokeo ya uchaguzi mkuu. Msemaji wa ikulu Manoah Esipisu wa ikulu  ametaja madai hayo kama propaganda zisizo na ukweli zinazolenga kuzua uhasama nchini. Katika taarifa, Esipisu amesisitiza msimamo wa rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto kwamba watakubali na kuheshimu matokeo ya uchaguzi kinyume na madai ya Raila. Amemtaka Raila na wenzake kuelezea taifa wako tayari kukubali matokeo ya uchaguzi bila kuweka vikwazo vinavyohatarisha kuandaliwa uchaguzi huo.

Show More

Related Articles