HabariMilele FmSwahili

NCIC yatoa majina ya watu wanaoeneza chuki mitandaoni

Tume ya uwiano na utangamano NCIC leo imetoa majina ya watu wanaodaiwa kueneza jumbe za chuki kwenye mitandao ya kijamii nchini. Mwenyekiti Francis Ole Kaparo amesema tume hiyo itahakikisha wahusika wanaadhibiwa vikali kisheria. Hatua ya NCIC inajiri wakati tume hiyo ikikabiliwa na maswali magumu kuhusu uwezo wake kuhakikisha wanaochochea umma wanachukuliwa hatua. Kaparo hata hivyo ameshikilia kuwa tume hiyo iko imara kutimiza wajibu wake.

Show More

Related Articles