HabariMilele FmSwahili

Wafanyibiashara Garissa waitaka serikali kutatua tatizo la uhaba wa unga

Wenye maduka katika kaunti ya Garisa wanaitaka serikali kukabili tatizo la uhaba wa unga wa mahindi mjini Garisa. Wafanyibiashara hao wanasema kiwango cha unga kinachowasilishwa mjini humo kwa sasa hakitoshelezi mahitaji ya wenyeji.  Kampuni za kusaga mahindi aidha zimeamua  kuagiza mahindi kutoka nchi jirani ya Ethiopia hali inayowalazimu kuongeza bei ya unga kwa hadi shilingi 132.

Show More

Related Articles