HabariMilele FmSwahili

NASA kuwasilisha rufaa dhidi ya uamuzi wa IEBC kubatilisha kandarasi ya uchapishaji karatasi za kura ya urais

Muungano wa upinzani NASA, unapanga kuwasilisha rufaa dhidi ya uamuzi wa tume ya uchaguzi kupinga uamuzi wa kubatilisha kandarasi ya uchapishaji karatasi za kura ya urais. Jaji wa mahakama ya rufaa Paul Kihara hata hivyo ameagiza mawakili kutoka pande zote ikiwemo NASA, na IEBC kuwasilisha mapendekezo yao kortini kufikia kesho. Kesi hiyo sasa itaskizwa Ijumaa hii na jopo la majaji watano. Mawakili wa IEBC wakiongozwa na wakili Paul Muite hata hivyo wameapa kupinga rufaa itakayowasilishwa na NASA hadi ile ya IEBC itakaposkizwa na uamuzi kutolewa.

Show More

Related Articles