HabariPilipili FmPilipili FM News

Jubilee Yawaonya Wanaopanga Kuiba Kura Mombasa.

Chama cha Jubilee kimetoa hakikisho ya kulinda kura zake haswa za kaunti ya Mombasa huku kikiwatahadharisha baadhi ya wanasiasa wenye lengo la kuiba kura kwenye uchaguzi mkuu wa mwezi Agosti.

Akizungumza na wafanyibiashara katika soko la Kongowea,Mbunge wa Gatundu kusini Mose Kuria amemshtumu gavana wa kaunti ya Mombasa Ali Hassan Joho kwa kuendeleza siasa za vitisho wakati tarehe ya uchaguzi ikikaribia.

Kwa upande wake anaewania wadhfa wa ugavana kaunti ya Mombasa kwa tiketi ya Jubilee Suleiman Shahbal amewakashifu viongozi wanaoendeleza siasa za kikabila na uchochezi huku akisistiza kuwa yeyote anaeishi kaunti ya Mombasa anahisabika kama mtu wa Pwani.

 

 

Show More

Related Articles