HabariPilipili FmPilipili FM News

Gavana Joho Aungwa Mkono Na Jamii Ya Waluo Mombasa.

Jamii ya waluo imepinga vikali maneno ya baadhi yao ambao wanadai kutengwa na serikali ya kaunti ya Mombasa.

Akiongea kwa niaba ya kamati kuu ya utamaduni wa jamii ya waluo Reuben sidika amesema wao kama jamii wanaunga mkono gavana wa Mombasa Ali hassan joho, huku wakipuuzilia mbali baadhi yao ambao walimuidhinisha Hassan Omar Sarai hapo jana, wakisema hao lengo lao ni kujinufaisha kisiasa.

Kauli yao inajiri wakati jamii ya wakamba pia jamii ya wakamba ikiwa imemuidhinisha mgombea ugavana kwa tiketi ya chama cha wiper hassanOmar Sarai.

Show More

Related Articles