HabariMilele FmSwahili

Afisa wa polisi atafuta msaada wa mganga kuwanasa majambazi Nyeri

Wenyeji wa kijiji cha Kaagati  huko Mathira kaunti ya Nyeri wamestaajabishwa na hatua ya afisa mmoja wa polisi aliyetafuta msaada wa mganga wa kienyeji kunasa washukiwa wa ujambazi. Afisa huyo alikabidhiwa jogoo ambaye amekuwa kwenye jengo lake la kibiashara kwa muda wa siku nne baada ya kuahidiwa kuwa angewanasa washukiwa hao wanaomwangaisha. Afisa huyo alitakiwa kutompa chochote jogoo anayetarajiwa sasa kuwanasa washukiwa katika muda wa siku mbili.

Show More

Related Articles