HabariMilele FmSwahili

Rais na naibu wake wapuuza madai yakuwatenga wananchi wa maeneo Nyanza

Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto wamepuuza madai serikali ya Jubilee imewatenga wananchi wa maeneo yanayodhaniwa kuwa ngome ya upinzani. Wakiwahutubia wenyeji wa Homa Bay na Kisumu, rais na naibu wake wamesema Jubilee imewahudumia wakenya wote bila ubaguzi kwa miaka minne iliopita kwa kufanikisha miradi tofauti. Wakiongea baada ya kuzindua daraja la Mbita-Rusinga kwa gharama ya shilingi bilioni 1.5 na barabara ya viongozi hao wamesema wataendeleza ajenda yao ya maendeleo. Viongozi hao ambao baadaye wamezindua ujenzi wa kiwanda cha kutengeza vileo kwa gharama ya shilingi bilioni 15 wamewaomba wenyeji kuunga mkono Jubilee Agosti nane na kupiga kura kwa amani.

Show More

Related Articles