HabariPilipili FmPilipili FM News

Wanasiasa Wahimizwa Kukubali Matokea Ya Uchaguzi Wa Agosti.

Wanasiasa wametakiwa kukubali matokea ya uchaguzi yatakayotangazwa na tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC  baada ya uchaguzi wa agosti nane.

Wakiongea wakati wa kongamano la amani lilowahusisha wakuu wa usalama kutoka kaunti ya Mombasa na viongozi wa dini kwa kauli moja wametoa wito kwa viongozi wa kisiasa kukubali matokea ya uchaguzi na pia kuhubiri amani msimu huu wa sisa.

Hamisi libondo mmoja wa viongozi wa dini Mombasa ametoa kauli hio  huku akisistiza umoja wa wananchi na viongozi.

Wakati huohuo naibu kamishna wa kaunti ya Mombasa Rashid Were ametoa hakikisho kuwa maafisa wa polisi wataongezwa ili kuhakikisha usalama unadumishwa wakati huu wa kampeni za kisisa

Show More

Related Articles