HabariMilele FmSwahili

Polycarp Igathe amshtumu Kidero kwa kuchelewesha mishahara ya wafanyikazi wa kaunti ya Nairobi

Mgombea mwenza wa seneta wa Nairobi Mike Sonko Polycarp Igathe  amemshtumu gavana wa sasa Evans Kidero kwa kuchelewesha mishahara ya wafanyikazi wa kaunti. Igathe amesema ni aibu kwa wafanyikazi wa kaunti kutishia  kugoma kwa kukosa kulipwa mishahara yao. Akiongea baada ya kukutana na wauguzi wa kaunti wanaogoma, Igathe ameahidi kutatua shida zao iwapo seneta Sonko atatwaa ushindi Agosti 8. Wakati huo huo,seneta mteule Beatrice Elachi aliyeandamana na Igathe ameitetea kauli ya raisi Uhuru Kenyatta kwamba upinzani unapania kuhujumu tume ya IEBC kwa kutumia mahakama.

Show More

Related Articles