HabariMilele FmSwahili

Kabogo aitaka serikali kuongeza faini inayotozwa wachafuzi wa mazingira

Gavana wa Kiambu William Kabogo sasa anaitaka serikali kuongeza faini inayotozwa wanaohusika katika uchafuzi wa mazingira kutoka shulingi elfu 10 hadi milioni moja. Kabogo amesema hayo alipoongoza wakazi wa Gitambaya Ruiru katika maandamano kulalamikia kumwagwa bara barani kwa maji taka kutoka jengo moja eneo hilo. Kabogo ametoa makataa ya siku tatu wapangaji wa jengo hilo kuhama huku akifutilia mbali leseni yake. Kabogo pia ameunga mkono uamuzi wa tume ya SRC kupunguza mishahara ya watumishi wa umma

Show More

Related Articles