HabariMilele FmSwahili

Ujumbe wa wakuu wa usalama kuzuru nyumbani kwa mwendazake Nkaiserry

Ujumbe wa wakuu wa usalama nchinui unazuru nyumbani kwa mwendazake generali mstaafu Joseph Nkaissery eneo la Karen. Ujumbe huo unaongozwa na inspecta generali wa polisi Jospeh Boinett,katibu wa usalama Karanja Kibicho na mkurugenzi wa jinai Ndegwa Muhoro. Wakuu hao aidha wanalenga kuifariji familia hiyo ya aliyekuwa mkuu wao kazini. Misa ya wafu kwa ajili ya mwendazake itaandaliwa kesho alasiri  katika kanisa la Nairobi Baptist huku mazishi yake generali mstaafu Nkaissery ikiandaliwa Jumamosi hii nyumbani kwake eneo la Il bisil Kajiado.

Show More

Related Articles