HabariMilele FmSwahili

Mahakama ya rufaa kutoa mwelekeo kuhusiana na kesi ya uchapishaji wa karatasi za kura

Majaji wa mahakama ya rufaa wakiongozwa naye Paul Kihara wanatarajiwa kutoa mwelekeo wao leo kuhusiana na rufaa iliyowasilishwa na tume ya uchaguzi na mipaka kupinga kubatilishwa kandarasi ya uchapishaji karatasi za kura ya urais. Kwenye rufaa hiyo, IEBC inasema jopo la majaji Joel Ngugi. J.J Mativo na George Odunga lilikwenda kinyume na katiba kwa kutumia suala la kuhusisha umma, kuamua IEBC haikufaa kuipa Alghurair kandarasi hiyo. Chebukati ana imani mahakama itaangazia masuala tata ambayo wameyawasilisha.rufaa hiyo itasikizwa mbele ya jopo la majaji 5 ijumaa hii.

Show More

Related Articles