HabariMilele FmSwahili

Wafanyikazi Transnzoia watishia mgomo iwapo hawatalipwa mishahara yao

Wafanyikazi wa serikali ya kaunti ya Trans Nzoia watoa makataa ya jumaa moja kwa serikali hio kuwalipa mishahara na malimbikizi ya mishahara yao au waandae mgomo. Wafanyikazi hao kupitia mwavuli wa chama cha wafanyikazi wa kaunti chini ya kiongozi Eliud Navimba, wamelalamikia kutolipwa mishahara ya zaidi ya mwezi mmoja wakidai fedha hizo zimetumiwa kuwalipa wanakadarasi. Eliud Navimba ni kiongozi wao. Kwa sasa wanatishia kusabaratisha utoaji wa huduma iwapo hawatalipwa fedha zao huku serikali hio bado ikikumbwa na mgomo wa wahudumu wa afya.

Show More

Related Articles