HabariMilele FmSwahili

Wakongwe wote kaunti ya Baringo kupata fedha za kujikimu

Serikali imeweka mikakati ya kuwawezesha wakongwe wote wa miaka 70 kujisajili ili kupokea fedha za kujikimu kutoka serikali kuu kila mwezi chini ya mpango wa inua jamii. Akizungumza baada ya kuzindua  usajili wa wakongwe katika kaunti ya Baringo waziri wa leba Philis Kandie amesema wakongwe watahitajika kuwasilisha vitambulisho vyao pekee ili kusajiliwa. Amesema serikali inanuia kuwasajili wakongwe nusu milioni kote nchini kabla ya mpango huo kukamilika tarehe 31 mwezi huu. Pia amewataka machifu kusimamia fedha hizo vyema na kuhakikisha zinawafika walenngwa watakaoanza kuzipokea januari mwaka ujao.

Show More

Related Articles