HabariMilele FmSwahili

Serikali kuwaajiri vijana vijana 45 000 kupitia shirika la NYS

Serikali itawaajiri vijana 45,000 kila mwaka chini ya mpango wa ajira kupitia shirika la huduma kwa vijana. Waziri wa jinsia na masuala ya vijana Cecil Kariuki anasema idadi hii itaongezeka kutoka 4000 ambao wanaajiriwa kwa sasa kila mwaka. Akiongea huko Mbeere kaskazini ambako alizindua mradi uliofadhilwia na mpango wa NYS, waziri huyo amesema vijana watasajiliwa mara tatu kwa mwaka ili kufikia idadi hiyo. Mpango huu utanza kutekelezwa mwezi huu.

Show More

Related Articles