MichezoPilipili FmPilipili FM News

James Rodriguez Ajiunga Na Bayern Munich

Kiungo mshambulizi kutoka Columbia James Rodriguez amejiunga rasmi na kilabu ya Bayern Munich kutoka Real Madrid kwa mkataba wa mkopo wa miaka miwili na kuna uwezekano wa kilabu la Bayern kumsajili kwa mkataba wa kudumu.

Mshambulizi huyo alikuwa akinyatiwa na vilabu vya PSG, Manchester United pamoja na Chelsea lakini sasa ameamua kujiunga na miamba hiyo ya ujerumani.

Miamba hiyo ya ujerumani inaweza kuruhusiwa kumsajili kwa mkataba wa kudumu kama watatoa pauni milioni 45.

Rais wa Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge amethibitisha usajili huo na kumsifia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25.

Show More

Related Articles