HabariMilele FmSwahili

Wakenya watakiwa kukoma kuweka ujumbe usiofaa kuhusu Nkaiserry mitandaoni

Wakenya wametakiwa kukoma kuweka jumbe zisizofaa kuhusiana na kifo cha aliyekuwa waziri wa usalama wa ndani Joseph Nkaissery kwenye mitandao ya kijamii. Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mazishi yake waziri Cleopa Mailu anasema jumbe hizo zimekuwa zikikera familia ya mwendazake. Mailu anasema licha ya kuheshimu Uhuru wa kujieleza wakenya wanastahili kuweka jumbe zinazofaa. Anasema jumbe hizo zimekuwa zikilenga kuchochea umma. Anasema matokeo ya upasuaji tayari yamebaini kuwa marehemu alifariki kutokana na mshtuko wa moyo. Anasema kamati yake imeridhishwa na matokeo hayo ya upasuaji.

Show More

Related Articles