HabariMilele FmSwahili

Wachuuzi wa maji Nairobi kuelezea wanakotoa maji hayo

Wachuuzi wa maji kaunti ya Nairobi watalazimika kuelezea wanakotoa maji hayo kuanzia leo. Hii ni kufuatia agizo la waziri wa afya kaunti ya Nairobi Benard Muia kutaka ukaguzi wa bidhaa hiyo. Muia anasema maji chafu yanayouziwa wenyeji yamechangia zaidi visa vya kipindu pindu. Ameagiza pia maafisa hao kuhakikisha wanaochuuza vyakula wameidhinishwa kisheria. Wakati huo huo Muia ameshtumu wauguzi wanaogoma kwa kupuuza majukumu yao ya kulinda maisha na kulenga kujinufaisha kifedha.

Show More

Related Articles