HabariMilele FmSwahili

Jubilee kutoshiriki mkutano wa kuamua kampuni ya kuchapisha karatasi za kupigia kura

Jubilee haitashiriki mkutano wowote kuamua kampuni itakayochapisha karatasi za kupigia kura za urais. Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto wanasema ni jukumu la tume ya IEBC kukabidhi kampuni wanayotaka ichapishe karatasi hizo wala sio jukumu la Jubilee. Wakiongea huko Narok,viongozi wamesema Jubilee iko tayari kwa uchaguzi wa Agosti nane bila kujali iwapo ni upinzani au IEBC itaamua atakayechapisha karatasi hizo.Aidha viongozi hao wamekashifu upinzani kwa kutaka ya kutatiza uchaguzi wakiwarai wakenya kujitokeza kwa wingi Agosti nane na kuichagua Jubilee kuendelea na kazi ya kulihudumia taifa.

Show More

Related Articles