HabariPilipili FmPilipili FM News

Nicholas Biwott Amefariki Dunia.

Mwanasiasa maarufu ambaye pia aliwai kuwa waziri katika serikali ya mstaafu Daniel Arap Moi, Nicholas Biwot amefariki dunia.

Biwot amefariki katika hospitali ya Nairobi mapema leo, wakati akifanyiwa uchunguzi wa kiafya baada ya kuhisi vibaya ghafla.

Taarifa zaidi zinaashiria kuwa kiongozi huyo amekuwa akiugua kwa mda.

Biwot aliwai kuhudumu kama mbunge wa keiyo kusini kwa miaka 28, baada ya kuchaguliwa mwaka wa 1974 hadi disemba mwaka wa 2007.

Bewot ambaye amefariki akiwa na miaka 75, hivi karibuni alitangaza azma yake ya kuunga mkono kuteuliwa kwa serikali ya jubilee kwa muhula wa pili.

 

Show More

Related Articles