HabariMilele FmSwahili

Viongozi wa kidini TanaRiver kukata rufaa dhidi ya marufuku ya kutotoka nje

Viongozi wa kidini kaunti ya Tana River wameapa kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa serikali kujumuisha kaunti ya Tana River miongoni mwa kaunti zilizowekea marufuku ya kutotoka nje kutokana na mashambulizi ya kigaidi. Wakiongozwa na mwenyekiti wa baraza la wahubiri na maimam huko Tana River Sheikh Musa  wanasema hakujakuwa na visa vyovyote vya ugaidi katika kaunti hiyo. Anasema kwa sasa hakuna dalili zozote za utovu wa usalama kaunti hiyo licha ya kuwa uchaguzi unakaribia mwezi ujao.

Show More

Related Articles