HabariPilipili FmPilipili FM News

Rais Kenyatta Aunga Mkono Hatua Ya Kukatwa Mishahara Kwa Wafanyikazi Wa Umma.

Rais uhuru Kenyatta ameunga mkono hatua ya tume ya mishahara na marupurupu nchini kupunguza mishahara ya wafanyikazi wa umma.

Akiongea huko ikulu mapema leo rais ameipongeza tume ya SRC akisema hatua yake inaendana na azimio la serikali ya jubilee katika kupunguza gharama na matumizi ya serikali.

Rais Kenyatta amewataka wakenya na maafisa wote wa umma kuukumbatia mpango huo, akisema pesa nyingi zitakazo kusanywa zitasaidia kutekeleza miradi muhimu kwa wananchi.

Aidha ametaka mpango huo uendeshwe kwa usawa kwa maafisa  wote wa umma bila upendeleo.

Baadhi ya wananchi wameunga mkono hatua hiyo huku wakipendekeza mishahara hiyo ipunguzwe hata zaidi, kwa kuwa bado iko juu kulingana na gharama ya maisha kwa mwananchi wa chini.

Show More

Related Articles