HabariPilipili FmPilipili FM News

Badi Atishia Kumshtaki Marwa.

Mbunge wa Jomvu Badi Twalib amepinga madai yaliotolewa na mshirikishi wa serikali kuu kanda ya Pwani Nelson Marwa ya kuunda makundi ya vijana katika eneo hilo kwa nia ya kuvuruga amani wakati wa uchaguzi.

Akizungumza alipokuwa akiwahutubia wanahabari,Badi amemtaka Marwa kuja na ushahidi kamili kuhusiana na madai hayo huku akitishia kumfungulia mashtaka.

Kauli ya Badi inajiri baada ya Marwa kumshtumu mbunge huyo kwa kuajiri vijana kuzua rabsha wakati huu wa siasa pamoja na kuharibu mradi wa srikali wa SGR.

Show More

Related Articles