HabariMilele FmSwahili

Baraza la magavana lawataka wanasiasa kuheshimu idara ya mahakama

Baraza la magavana limewataka wanasiasa nchini kuheshimu uhuru wa idara ya mahakama na maamuzi inayotoa. Naibu mwenyekiti wa baraza la magavana John Mrutu ameonya dhidi ya kukashifiwa kwa maamuzi yanayotolewa na majaji. Amesema mvutano unaoendelea kati ya muungano wa NASA na Jubilee kuhusu kandarasi ya kuchapisha karatasi za kupigia kura ni ishara kuwa baadhi ya wanasiasa wanalenga kuhujumu utenda kazi wa mahakama.

Show More

Related Articles