HabariMilele FmSwahili

Kenya yaadhimisha siku yakimataifa ya idadi ya watu duniani

Kenya inaungana na nchi zingine duniani kuadhimisha siku ya kimataifa ya idadi ya watu duniani. Hafla ya kitaifa inaendelea hivi sasa hapa jiini Nairobi. maadhimisho haya yanatumika kufahamu idadi kamili ya watu ili kuweka miakati mwafaka ya kimaendeleo. Shirika la umoja wa mataifa la idadi ya watu UNFP limeelezea haja ya kuimarisha juhudi za kuzihamasisha jamii katika maeneo mbali mbali nchini kupanga uzazi. Naibu mkurugenzi wa shirika hilo nchini Judith Kunyiha ametaja maeneo ya kaskazini mashariki kuwa na idadi ndogo zaidi ya watu ambao hawajakumbatia upangaji uzazi.

Show More

Related Articles