HabariMilele FmSwahili

Sudan yaitaka Marekani kuindolea vikwazo

Wawakilishi wa umoja wa mataifa nchini Sudan wameitaka marekani kuondoa vikwazo dhidi ya taifa hilo. Rais Trump ataamua kesho  iwapo vikwazo hivyo vilivyowekwa na Obama vitaongezwa au kuondolewa . Wawakilishi hao wamesema kuwa Sudan imeweza kutoa ulinzi na ushirikiano wa kutosha katika maeneo ambayo hayakufikika awali kutokana na vita. Baadhi ya wanaharakati wanasema kuwa kuiwekea vikwazo Sudan ni kuwaongezea matatizo wananchi wake na sio rais wa nchi hiyo Omar Al bashir

Show More

Related Articles