HabariMilele FmSwahili

Viongozi wa kisiasa waikosoa hatua ya SRC kupunguza mishahara ya wabunge

Baadhi ya viongozi wa kisiasa wameonya kuwa hatua ya tume ya SRC kupunguza mishahara ya watumishi wa umma itaathiri utendakazi wa wabunge nchini. Mbunge wa Yatta Francis Mwangangi anasema wabunge huenda wakasusia baadhi ya vikao kwa kukosa marupu rupu. Kauli sawa imetolewa na mbunge wa kamukunji Yusuf Hassan. Naye afisa mkuu wa muungano wa NASA Norman Magaya ameikosoa tume ya SRC kwa kutofanya mashauriano kabambe kabla ya kutangaza ratiba mpya ya mishahara

Show More

Related Articles