HabariMilele FmSwahili

Wanasheria nchini waitetea idara ya mahakama

Wanasheria nchini wanaendelea kuitetea idara ya mahakama dhidi ya kile kimetajwa kuwa kushambuliwa na wanasiasa. Chama cha mawakili LSK, kanda ya south rift kimewaonya wanasiasa dhidi ya
kuwashambulia majaji na mahakimu kwenye mikutano ya kisiasa.Kwa mujibu wa mwenyekiti wa LSK kanda hiyo Erastus Orina, hulka hiyo inaweza kuondoa imani ya wakenya katika idara ya mahakama.Amewataka  wasioridhika na maamuzi ya mahakama kufuata sheria zilizopo.

Show More

Related Articles