HabariMilele FmSwahili

Jubilee kupeleka kampeini zake kaunti ya Narok

Rais Uhuru Kenyatta leo anaongoza kampeni za chama cha Jubilee katika kaunti ya Narok. Rais  na naibu wake William Ruto wanatarajiwa kuwasili eneo la Olemekenyu Narok kusini saa nne asubuhi ambako watahutubia mkutano wa kisiasa. Pia watazuru Ilmotiok na Oloolaimutia katika eneo la Narok Magharibi. Aidha wameratibiwa kuzindua mradi wa bara bara ya Mau Narok na pia kutoa hati miliki za mashamba kwa wenyeji huko Narok kusini. Baadaye rais Kenyatta na naibu wake watazuru shule ya upili ya wasichana ya Maasai kutoa basi la shule kabla ya kuhutubia mkutano katika uwanja wa Narok. Wenyeji wameelezea imani kuwa ziara hiyo itafanikisha maendeleo katika kaunti ya Narok

Show More

Related Articles