HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

SRC imetoa mpangilio mpya wa mishahara serikalini

Mtumishi wowote wa umma atayeajiriwa kuanzia sasa atapokea mshahara mpya uliopunguzwa baada ya kuratibiwa na tume ya kuratibu mishahara SRC.
Mishahara ya watumishi wote wa umma itapunguzwa baada ya uchaguzi mkuu ujao.
Ratiba ya hivi punde ya tume ya kuratibu mishahara ya wafanyikazi wa umma SRC inaashiria rais atapokea shilingi milioni 1.44 kutoka milioni 1.6 huku naibu wake akipokea shilingi milioni 1.2 kutoka milioni 1.4.
SRC pia imefutilia mbali marupurupu yote ya magavana, na yale ya usafiri na kuhudhuria vikao vya bunge kwa maseneta na wabunge, ili kuhifadhi shilingi bilioni 8.8 zinazotumika zaidi kugharamia mishahara ya watumishi hao.

Show More

Related Articles