HabariPilipili FmPilipili FM News

Mbogo Amlaumu Bedzimba Kwa Utovu Wa Usalama Kisauni.

Mwaniaji wa kiti cha ubunge eneo la Kisauni Ali Mbogo amelaumu uongozi wa mbunge wa sasa Rashid Bdzimba kutokana na visa vya utovu wa usalama eneo hilo.

Akiongea na meza yetu ya habari Mbogo amesifia uongozi wa wabunge wa  zamani kama vile Anania Mwaboza , Ali Hassan JOHO na marehemu  Karisa Maitha.

Kiongozi huyo ameeleza kuwa vijana wengi hujiunga na makundi ya kigaidi kutokana na wao kukosa pesa za kufadhili masomo ya kiufundi .

Aidha Mbogo amelaumu uongozi wa sasa kwa ukosefu wa vyuo vya kiufundi eneo la kisauni.

Wakati huo huo ametaja matumizi ya mihadarati kama chanzo kikuu cha ukosefu wa usalama katika mitaa ya kisauni.

Show More

Related Articles