HabariMilele FmSwahili

Wabunge wapata pigo baada ya SRC kufutilia mbalimbali marupurupu yao

Wabunge wamepata pigo baada ya tume ya kuangazia mishara ya umma kufutilia mbali marupurupu waliokuwa wakipata katika bunge la kitaifa na lile la seneti. SRC imeondoa marupurupu ya vikao vya bunge usafiri na yale marupurupu ya kutekeleza majukumu spesheli. Rais na maafisa wengine  wa umma hawakusazwa baada ya kupunguzwa kwa mishahara wanayopata kila mwezi huku rais atakayechaguliwa Agosti nane sasa akitarajiwa kupata mshahara wa shilingi milioni 1.4 kinyume na milioni 1.6  ilivyo sasa. Serem amesema  hatua hiyo itapelekea taifa kuokoa  shilingi bilioni 8, milioni 853 elfu 204 na 952.

Show More

Related Articles