HabariMilele FmSwahili

SRC yajiondolea lawama kutokana na mgomo wa wauguzi

Tume ya SRC  imejiondolea lawama kutokana na mgomo wa wauguzi unaoendelea kwa sasa. Mwenyekiti wa SRC Sarah Serem anasema kundi lililobuniwa kushughulikia mkataba wa  wauguzi kwa ushirikiano na waajiri wa wauguzi kuangazia gharama itakayotumika. Serem anasema kwa sasa wanasubiri ripoti kutoka kwa baraza la magavana kubaini iwapo wana uwezo wa kumudu gharama  ya mkataba wao na wauguzi ya shilingi bilioni 40. Nao wauguzi hao walioshiriki mgomo hadi afisi za SRC wakiongozwa na naibu katibu Maurice Opetu wameapa kutorejea kazini hadi pale matakwa yao yatakapoangaziwa.

Show More

Related Articles